Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 99 (Sura 99)
1; Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!
2; Na itakapo toa ardhi mizigo yake!
3; Na mtu akasema: Ina nini?
4; Siku hiyo itahadithia khabari zake.
5; Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!
6; Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!
7; Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona!
8; Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!

Pages ( 99 of 114 ): « Previous1 ... 9798 99 100101 ... 114Next »