Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 88 (Sura 88)
1; Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?
2; Siku hiyo nyuso zitainama,
3; Zikifanya kazi, nazo taabani.
4; Ziingie katika Moto unao waka –
5; Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.
6; Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba.
7; Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.
8; Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.
9; Zitakuwa radhi kwa juhudi yao,
10; Katika Bustani ya juu.
11; Hawatasikia humo upuuzi.
12; Humo imo chemchem inayo miminika.
13; Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa,
14; Na bilauri zilizo pangwa,
15; Na matakia safu safu,
16; Na mazulia yaliyo tandikwa.
17; Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
18; Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?
19; Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?
20; Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?
21; Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
22; Wewe si mwenye kuwatawalia.
23; Lakini anaye rudi nyuma na kukataa,
24; Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!
25; Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.
26; Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!

Pages ( 88 of 114 ): « Previous1 ... 8687 88 8990 ... 114Next »