Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 1 (Sura 1)
1; KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
2; Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;
3; Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;
4; Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo.
5; Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.
6; Tuongoe njia iliyo nyooka,
7; Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.

Pages ( 1 of 114 ): 1 23 ... 114Next ยป