Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 78 (Sura 78)
1; WANAULIZANA nini?
2; Ile khabari kuu,
3; Ambayo kwayo wanakhitalifiana.
4; La! Karibu watakuja jua.
5; Tena la! Karibu watakuja jua.
6; Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko?
7; Na milima kama vigingi?
8; Na tukakuumbeni kwa jozi?
9; Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko?
10; Na tukaufanya usiku ni nguo?
11; Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha?
12; Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu?
13; Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto;
14; Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni,
15; Ili tutoe kwayo nafaka na mimea,
16; Na mabustani yenye miti iliyo kamatana.
17; Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake,
18; Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi,
19; Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango,
20; Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi.
21; Hakika Jahannamu inangojea!
22; Kwa walio asi ndio makaazi yao,
23; Wakae humo karne baada ya karne,
24; Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji,
25; Ila maji yamoto sana na usaha,
26; Ndio jaza muwafaka.
27; Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu.
28; Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu.
29; Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika.
30; Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu!
31; Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu,
32; Mabustani na mizabibu,
33; Na wake walio lingana nao,
34; Na bilauri zilizo jaa,
35; Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo –
36; Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha.
37; Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake!
38; Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu.
39; Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi.
40; Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo!

Pages ( 78 of 114 ): « Previous1 ... 7677 78 7980 ... 114Next »