Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 101 (Sura 101)
1; Inayo gonga!
2; Nini Inayo gonga?
3; Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?
4; Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;
5; Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!
6; Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
7; Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
8; Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,
9; Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!
10; Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?
11; Ni Moto mkali!

Pages ( 101 of 114 ): « Previous1 ... 99100 101 102103 ... 114Next »