Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 82 (Sura 82)
1; Mbingu itapo chanika,
2; Na nyota zitapo tawanyika,
3; Na bahari zitakapo pasuliwa,
4; Na makaburi yatapo fukuliwa,
5; Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma.
6; Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?
7; Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha,
8; Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga.
9; Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo.
10; Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu,
11; Waandishi wenye hishima,
12; Wanayajua mnayo yatenda.
13; Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema,
14; Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni;
15; Wataingia humo Siku ya Malipo.
16; Na hawatoacha kuwamo humo.
17; Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
18; Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
19; Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.

Pages ( 82 of 114 ): « Previous1 ... 8081 82 8384 ... 114Next »