Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 107 (Sura 107)
1; Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo?
2; Huyo ndiye anaye msukuma yatima,
3; Wala hahimizi kumlisha masikini.
4; Basi, ole wao wanao sali,
5; Ambao wanapuuza Sala zao;
6; Ambao wanajionyesha,
7; Nao huku wanazuia msaada.

Pages ( 107 of 114 ): « Previous1 ... 105106 107 108109 ... 114Next »