Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 93 (Sura 93)
1; Naapa kwa mchana!
2; Na kwa usiku unapo tanda!
3; Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
4; Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
5; Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
6; Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
7; Na akakukuta umepotea akakuongoa?
8; Akakukuta mhitaji akakutosheleza?
9; Basi yatima usimwonee!
10; Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!
11; Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.

Pages ( 93 of 114 ): « Previous1 ... 9192 93 9495 ... 114Next »