Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 95 (Sura 95)
1; Naapa kwa tini na zaituni!
2; Na kwa Mlima wa Sinai!
3; Na kwa mji huu wenye amani!
4; Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.
5; Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!
6; Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha.
7; Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo?
8; Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?

Pages ( 95 of 114 ): « Previous1 ... 9394 95 9697 ... 114Next »