Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 94 (Sura 94)
1; Hatukukunjulia kifua chako?
2; Na tukakuondolea mzigo wako,
3; Ulio vunja mgongo wako?
4; Na tukakunyanyulia utajo wako?
5; Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi,
6; Hakika pamoja na uzito upo wepesi.
7; Na ukipata faragha, fanya juhudi.
8; Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.

Pages ( 94 of 114 ): « Previous1 ... 9293 94 9596 ... 114Next »