Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 90 (Sura 90)
1; Naapa kwa Mji huu!
2; Nawe unaukaa Mji huu.
3; Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa.
4; Hakika tumemuumba mtu katika taabu.
5; Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza?
6; Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.
7; Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?
8; Kwani hatukumpa macho mawili?
9; Na ulimi, na midomo miwili?
10; Na tukambainishia zote njia mbili?
11; Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.
12; Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani?
13; Kumkomboa mtumwa;
14; Au kumlisha siku ya njaa
15; Yatima aliye jamaa,
16; Au masikini aliye vumbini.
17; Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.
18; Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.
19; Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni.
20; Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.

Pages ( 90 of 114 ): « Previous1 ... 8889 90 9192 ... 114Next »