Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 86 (Sura 86)
1; Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!
2; Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku?
3; Ni Nyota yenye mwanga mkali.
4; Hapana nafsi ila inayo mwangalizi.
5; Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?
6; Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,
7; Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.
8; Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha.
9; Siku zitakapo dhihirishwa siri.
10; Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.
11; Naapa kwa mbingu yenye marejeo!
12; Na kwa ardhi inayo pasuka!
13; Hakika hii ni kauli ya kupambanua.
14; Wala si mzaha.
15; Hakika wao wanapanga mpango.
16; Na Mimi napanga mpango.
17; Basi wape muhula makafiri – wape muhula pole pole.

Pages ( 86 of 114 ): « Previous1 ... 8485 86 8788 ... 114Next »