Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 81 (Sura 81)
1; Jua litakapo kunjwa,
2; Na nyota zikazimwa,
3; Na milima ikaondolewa,
4; Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe,
5; Na wanyama wa mwituni wakakusanywa,
6; Na bahari zikawaka moto,
7; Na nafsi zikaunganishwa,
8; Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa,
9; Kwa kosa gani aliuliwa?
10; Na madaftari yatakapo enezwa,
11; Na mbingu itapo tanduliwa,
12; Na Jahannamu itapo chochewa,
13; Na Pepo ikasogezwa,
14; Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha.
15; Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma,
16; Zinazo kwenda, kisha zikajificha,
17; Na kwa usiku unapo pungua,
18; Na kwa asubuhi inapo pambazuka,
19; Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu,
20; Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi,
21; Anaye t´iiwa, tena muaminifu.
22; Na wala huyu mwenzenu hana wazimu.
23; Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi.
24; Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu.
25; Wala hii si kauli ya Shetani maluuni.
26; Basi mnakwenda wapi?
27; Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
28; Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa.
29; Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Pages ( 81 of 114 ): « Previous1 ... 7980 81 8283 ... 114Next »