Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 96 (Sura 96)
1; Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,
2; Amemuumba binaadamu kwa tone la damu,
3; Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
4; Ambaye amefundisha kwa kalamu.
5; Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.
6; Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri
7; Akijiona katajirika.
8; Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.
9; Umemwona yule anaye mkataza
10; Mja anapo sali?
11; Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu?
12; Au anaamrisha uchamngu?
13; Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?
14; Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?
15; Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!
16; Shungi la uwongo, lenye makosa!
17; Basi na awaite wenzake!
18; Nasi tutawaita Mazabania!
19; Hasha! Usimt´ii! Nawe sujudu na ujongee!

Pages ( 96 of 114 ): « Previous1 ... 9495 96 9798 ... 114Next »