Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 92 (Sura 92)
1; Naapa kwa usiku unapo funika!
2; Na mchana unapo dhihiri!
3; Na kwa Aliye umba dume na jike!
4; Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.
5; Ama mwenye kutoa na akamchamngu,
6; Na akaliwafiki lilio jema,
7; Tutamsahilishia yawe mepesi.
8; Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake,
9; Na akakanusha lilio jema,
10; Tutamsahilishia yawe mazito!
11; Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia?
12; Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu.
13; Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
14; Basi nakuonyeni na Moto unao waka!
15; Hatauingia ila mwovu kabisa!
16; Anaye kadhibisha na kupa mgongo.
17; Na mchamngu ataepushwa nao,
18; Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
19; Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa.
20; Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
21; Naye atakuja ridhika!

Pages ( 92 of 114 ): « Previous1 ... 9091 92 9394 ... 114Next »