Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 84 (Sura 84)
1; Itapo chanika mbingu,
2; Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
3; Na ardhi itakapo tanuliwa,
4; Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu,
5; Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
6; Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.
7; Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia,
8; Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi,
9; Na arudi kwa ahali zake na furaha.
10; Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake,
11; Basi huyo ataomba kuteketea.
12; Na ataingia Motoni.
13; Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.
14; Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.
15; Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!
16; Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,
17; Na kwa usiku na unavyo vikusanya,
18; Na kwa mwezi unapo pevuka,
19; Lazima mtapanda t´abaka kwa t´abaka!
20; Basi wana nini hawaamini?
21; Na wanapo somewa Qur´ani hawasujudu?
22; Bali walio kufuru wanakanusha tu.
23; Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria.
24; Basi wabashirie adhabu chungu!
25; Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika.

Pages ( 84 of 114 ): « Previous1 ... 8283 84 8586 ... 114Next »