Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 55 (Sura 55)
1; Arrah´man, Mwingi wa Rehema
2; Amefundisha Qur´ani.
3; Amemuumba mwanaadamu,
4; Akamfundisha kubaini.
5; Jua na mwezi huenda kwa hisabu.
6; Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea.
7; Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani,
8; Ili msidhulumu katika mizani.
9; Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani.
10; Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe.
11; Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba.
12; Na nafaka zenye makapi, na rehani.
13; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
14; Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo..
15; Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto.
16; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
17; Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili.
18; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
19; Anaziendesha bahari mbili zikutane;
20; Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane.
21; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
22; Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani.
23; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
24; Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima.
25; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
26; Kila kilioko juu yake kitatoweka.
27; Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.
28; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
29; Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo.
30; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
31; Tutakuhisabuni enyi makundi mawili.
32; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
33; Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka.
34; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
35; Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda.
36; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
37; Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta.
38; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
39; Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini.
40; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
41; Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu.
42; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
43; Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha.
44; Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka.
45; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
46; Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili.
47; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
48; Bustani zenye matawi yaliyo tanda.
49; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
50; Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita.
51; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
52; Humo katika kila matunda zimo namna mbili.
53; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
54; Wawe wameegemea matandiko yenye bit´ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu.
55; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
56; Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini.
57; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
58; Kama kwamba wao ni yakuti na marijani.
59; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha.
60; Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?
61; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
62; Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili.
63; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
64; Za kijani kibivu.
65; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
66; Na chemchem mbili zinazo furika.
67; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
68; Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga.
69; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
70; Humo wamo wanawake wema wazuri.
71; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
72; Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema.
73; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
74; Hajawagusa mtu wala jini kabla yao.
75; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
76; Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri.
77; Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
78; Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.

Pages ( 55 of 114 ): « Previous1 ... 5354 55 5657 ... 114Next »