Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 80 (Sura 80)
1; Alikunja kipaji na akageuka,
2; Kwa sababu alimjia kipofu!
3; Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?
4; Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?
5; Ama ajionaye hana haja,
6; Wewe ndio unamshughulikia?
7; Na si juu yako kama hakutakasika.
8; Ama anaye kujia kwa juhudi,
9; Naye anaogopa,
10; Ndio wewe unampuuza?
11; Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.
12; Basi anaye penda akumbuke.
13; Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa,
14; Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.
15; Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,
16; Watukufu, wema.
17; Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?
18; Kwa kitu gani amemuumba?
19; Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.
20; Kisha akamsahilishia njia.
21; Kisha akamfisha, akamtia kaburini.
22; Kisha apendapo atamfufua.
23; La! Hajamaliza aliyo muamuru.
24; Hebu mtu na atazame chakula chake.
25; Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,
26; Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,
27; Kisha tukaotesha humo nafaka,
28; Na zabibu, na mimea ya majani,
29; Na mizaituni, na mitende,
30; Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,
31; Na matunda, na malisho ya wanyama;
32; Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
33; Basi utakapo kuja ukelele,
34; Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye,
35; Na mamaye na babaye,
36; Na mkewe na wanawe –
37; Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.
38; Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,
39; Zitacheka, zitachangamka;
40; Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,
41; Giza totoro litazifunika,
42; Hao ndio makafiri watenda maovu.

Pages ( 80 of 114 ): « Previous1 ... 7879 80 8182 ... 114Next »