Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 85 (Sura 85)
1; Naapa kwa mbingu yenye Buruji!
2; Na kwa siku iliyo ahidiwa!
3; Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa!
4; Wameangamizwa watu wa makhandaki
5; Yenye moto wenye kuni nyingi,
6; Walipo kuwa wamekaa hapo,
7; Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini.
8; Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa,
9; Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu.
10; Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.
11; Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
12; Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.
13; Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena,
14; Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi,
15; Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu,
16; Atendaye ayatakayo.
17; Je! Zimekuwasilia khabari za majeshi?
18; Ya Firauni na Thamudi?
19; Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha.
20; Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka.
21; Bali hii ni Qur´ani tukufu
22; Katika Ubao Ulio Hifadhiwa.

Pages ( 85 of 114 ): « Previous1 ... 8384 85 8687 ... 114Next »