Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 100 (Sura 100)
1; Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
2; Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
3; Wakishambulia wakati wa asubuhi,
4; Huku wakitimua vumbi,
5; Na wakijitoma kati ya kundi,
6; Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
7; Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!
8; Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!
9; Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
10; Na yakakusanywa yaliomo vifuani?
11; Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!

Pages ( 100 of 114 ): « Previous1 ... 9899 100 101102 ... 114Next »