Swahili Quran | Soma Kurani

Chapter 104 (Sura 104)
1; Ole wake kila safihi, msengenyaji!
2; Aliye kusanya mali na kuyahisabu.
3; Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele!
4; Hasha! Atavurumishwa katika H´ut´ama.
5; Na nani atakujuvya ni nini H´ut´ama?
6; Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa.
7; Ambao unapanda nyoyoni.
8; Hakika huo utafungiwa nao
9; Kwenye nguzo zilio nyooshwa.

Pages ( 104 of 114 ): « Previous1 ... 102103 104 105106 ... 114Next »